Alichosema kocha wa Westham United Manuel Pellegrini dhidi ya mechi ya kesho itakayopigwa London Westham United watakapoialika Chelsea

Kocha wa West Ham Manuel Pellegrini anaamini kwamba mwanzo mzuri wa Chelsea katika Ligi kuu ya Uingereza imewapa Motisha sahihi kukabiliana nao.
.
.
Vilabu hivyo viwili vinakabiliana kesho katika dimba la London, ambapo West Ham wamesitisha mtiririko wa kupoteza mechi 4 mfululizo kwa kuifunga Everton 3-1 wiki iliyopita.
Chelsea wenyewe wapo kileleni baada ya kushinda mechi zao zote tano za mwanzo na siku ya Alhamisi walishinda mechi ya 6 katika mashindano yote baada ya kuifunga PAOK , 1-0.
.
. " Najua kwamba hapa London kuna dabi nyingi sana , lakini sisi tunacheza dabi yetu ya kwanza tukiwa nyumbani dhidi ya Chelsea, na wapo kileleni mwa msimamo kwahiyo hiyo ni motisha kubwa sana ya kujaribu kuwafunga."
.
. " Lakini itabidi pia tuwe makini sana kwenye kuzuia kwasababu wanahitaji nafasi ndogo sana eneo la robo tatu ya mwisho ya uwanja kukuadhibu." #sokaliveupdates
Post a Comment