kocha mkuu wa chelsea aomba muda zaidi kuijenga timu yake
Maurizio Sarri amekiri kwamba Chelsea inahitaji kuboresha zaidi daraja lao ili kuwafikia vinara Liverpool baada ya kupata sare ya 0-0 dhidi ya West Ham.
.
.
Vilabu hivyo viwili vilikuwa vinaenda sambamba lakini Chelsea walishindwa kwenda sawa na Liverpool , baada ya vijana wa Klopp kushinda 3-0 dhidi ya Southampton.
.
. "Liverpool wapo hatua ya mbele zaidi yetu - Tulianza kufanya kazi pamoja siku 35, 40 zilizopita."
.
. "Kwahiyo kwetu sisi nafikiri kwamba ni mapema sana . Ni lazima tujitume. Inabidi tuboreshe na labda baada ya mwaka mmoja tutakuwa kwenye daraja sawa na Liverpool." #sokaliveupdates
Post a Comment